- Ulazima wa mtu kumpendelea ndugu yake kile anachokipenda kwa nafsi yake. Kwa sababu kukanushwa imani kwa mtu ambaye hampendelei ndugu yake kile anachopenda yeye mwenyewe kunaonyesha ulazima wa hilo.
- Udugu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu uko juu zaidi kuliko udugu wa nasaba (ukoo), kwani haki yake ni wajibu.
- Katazo la maneno na vitendo vyote vinavyopingana na upendo huu, kama vile udanganyifu, kusengenya, husuda, na uadui dhidi ya mtu, au mali yake, au heshima yake.
- Kutumia baadhi ya maneno yanayotia hamasa ya kufanya matendo; kwa kauli yake "Kwa ndugu yake".
- Amesema Al-Kirmani, Mwenyezi Mungu amrehemu: Pia ni sehemu ya imani kuchukia kwa ndugu yake uovu anaouchukia kwa nafsi yake, na hili (Mtume) hakulitaja, kwa sababu kukipenda kitu kunalazimu kuchukia kinyume chake, hivyo kuacha kutolisema hilo inatosha.