- Ukubwa wa haki za jirani na uwajibu wa kulichunga hilo.
- Msisitizo juu ya haki za jirani kwa kutoa usia, hii inamaanisha ulazima wa kumkirimu na kujipendekeza kwake na kumtendea wema, na kumzuilia madhara, na kumtembelea wakati wa maradhi, na kumpongeza wakati wa furaha, na kumpa pole wakati wa msiba.
- Kila unavyozidi kuwa karibu mlango wa jirani ndivyo ambavyo haki yake inazidi kuwa na mkazo zaidi.
- Ukamilifu wa sheria katika yale iliyokuja nayo, katika yale yenye kuitengeneza jamii kama kumtendea wema jirani, na kumzuilia madhara.