- Wajibu wa muumini ni kuwavutia watu kwa Mwenyezi Mungu na kuwahamasisha katika kheri.
- Ni wajibu kwa mwenye kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu atazame kwa hekima namna sahihi ya kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu.
- Kutoa habari njema huleta furaha na watu kuelekea na kutulizana kwa mlinganiaji na yale anayowafundisha watu.
- Kuwatia ugumu watu husababisha kuwachukiza watu na kuwakimbiza, na kuyatia shaka maneno ya mfikishaji.
- Upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake nakuwa Yeye ameridhia kwao dini ya upole na sheria nyepesi.
- Wepesi ulioamrishwa ni ule uliokuja katika sheria.