Hakika upole hauwi ndani ya kitu isipokuwa hukipendezesha, na hautolewi ndani ya kitu ila hukichafua
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe kwake- mke wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anasimulia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika upole hauwi ndani ya kitu isipokuwa hukipendezesha, na hautolewi ndani ya kitu ila hukichafua".
Imepokelewa na Imamu Muslim
Ufafanuzi
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa upole na ulaini na utaratibu katika kauli na matendo huyazidishia mambo uzuri na ukamilifu na ubora, na mtu mwenye sifa hizi hakika anastahiki kupata hitajio lake.
Na kukosekana kwa upole huyatia aibu mambo na kuyatia sura mbaya na humkwamisha mtu kupata shida yake, na hata akiipata huipata kwa tabu.
Hadeeth benefits
Himizo la kujipamba na upole.
Upole humpamba mtu, nayo ni sababu ya kila heri katika mambo ya Akhera na Dunia.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others