- Inapendeza kuleta dhikri hii asubuhi na jioni; ili mwanadam ahifadhike kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu lisimfike balaa ghafla au madhara ya msiba au mfano wa hayo.
- Nguvu kubwa ya yakini kwa wema wa mwanzo kwa Mwenyezi Mungu na kuyasadikisha kwao yale aliyoyaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Miongoni mwa faida za kufanywa dhikri ziwe za asubuhi na ajioni ni kuondoa hali ya kughafilika kwa muislamu na kuvuta kwake picha endelevu kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kwa kadiri inavyokuwa imani ya mtajaji Mwenyezi Mungu na unyenyekevu wake na kuhudhurisha kwake moyo, pamoja na kutakasa nia na yakini ndivyo itakavyozidi kupatikana athari ya dhikri.