- Nikuwa kudumu katika kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wazi na kwa siri ni katika mambo makubwa yanayomuweka mtu karibu na Mola wake, na yenye manufaa makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Vitendo vyote viliwekwa ili kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na simamisha sala kwa kunikumbuka". Naye, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, amesema: "Kuizunguka Al-Kaaba na baina ya Safa na Marwah na kurusha mawe kulikusudiwa tu kumtaja Mwenyezi Mungu" Imepokelewa na Abu Daudi na Tirmidhiy.
- Al-Izzi bin Abdul Salam amesema katika Qawaid yake: Hadithi hii inaashiria kwamba malipo hayatokani na kiwango cha uchovu katika ibada zote, bali Mwenyezi Mungu Mtukufu anaweza kulipa zaidi kwa matendo madogo kuliko mengi, hivyo malipo yanatokana na tofauti za daraja katika utukufu.
- Al-Munawiy amesema katika Faidh al-Qadir: Hadithi hii inafasiriwa kuwa dhikri imekuwa bora kwa wale walioambiwa kuifanya, kwakuwa, na lau kama mtu shupavu na shujaa angeliambiwa kuifanya na yakapatikana manufaa katika Uislamu basi ingeitwa Jihadi, au tajiri ambaye mali yake inawanufaisha masikini, basi ingeitwa sadaka, au mtu mwenye uwezo wa kuhiji, basi ingeitwa Hija, au mtu mwenye wazazi wawili, basi ingeitwa wema kwa wazazi, na kupitia kwake inapatikana taufiki kati ya habari na habari.
- Dhikiri iliyokamilika zaidi ni ile ambayo ulimi umetamka ikiwa pamoja na mazingatio ya moyo, kisha ile iliyomo moyoni peke yake kama tafakuri, kisha inayokuwa kwa ulimi peke yake, na kila moja ina ujira, In shaa Allah.
- Muislamu kudumu na dhikiri zenye kuendana na hali mbali mbali kama asubuhi na jioni, na kuingia msikitini na nyumbani na chooni na wakati wa kutoka, na nyinginezo, hii inamfanya kuwa miongoni mwa wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi.