- Sunna ya kuomba dua hii katika sijida.
- Amesema Miriki: Na katika moja kati ya riwaya za Nasaai: Alikuwa akisema dua hii anapomaliza swala yake na akaelekea kitandani kwake.
- Sunna ya kumsifia Mwenyezi Mungu kwa sifa zake na kumuomba kwa majina yake yaliyothibiti katika Qur'ani na Sunna.
- Hapa kuna kumtukuza muumba wakati wa kurukuu na kusujudu.
- Inafaa kuomba ulinzi kupitia sifa za Mwenyezi Mungu, kama ambavyo inafaa kuomba ulinza kupitia dhati yake Yeye Aliyetakasika na kutukuka.
- Amesema Al-Khattwabi: Katika maneno haya kuna maana ya ndani sana, nayo: Nikuwa aliomba kinga kwa Mwenyezi Mungu amkinge kupitia radhi zake kutokana na hasira zake, na kwa salama yake dhidi ya adhabu zake, na ridhaa na hasira ni maneno mawili tofauti yanayokwenda sambamba, vile vile kusalimika na kuadhibiwa pia, alipofikia kumtaja ambaye hana kinyume chake ambaye ni Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alitaka kinga kutokana na Yeye kwake mwenyewe na si kwa mwingine, na maana yake: Ni kuomba msamaha dhidi ya mapungufu ya kutofikia wajibu wa haki stahiki katika kumuabudu, na kumtukuza. Na kauli yake: Sizidhibiti sifa juu yako: Yaani sina uwezo wala siwezi kuzifikia.