- Inapendeza kusoma dua hii asubuhi na jioni, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Uhitaji wa mja kwa Mola wake Mlezi katika hali zake na nyakati zake zote.
- Kilicho bora katika kusoma Adhkari, asubuhi ni kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuchomoza Jua mwanzo wa mchana, na baada ya Laasiri mpaka kabla ya kuzama, ikiwa atazisoma baada ya hapo, yaani: Asubuhi akazisoma baada ya Jua kunyanyuka itafaa, na hata akizisoma baada ya Adhuhuri itafaa pia, na akizisoma baada ya Magharibi itafaa, huo ndio wakati wa kufanya Adhkari.
- Mahusiano kati ya kauli yake "na kwako tutafufuliwa" na kusemwa asubuhi, kauli hii inamkumbusha kuhuishwa na kufufuliwa kukubwa pindi watapokufa watu na kufufuliwa siku ya Kiyama, huku ni kufufuliwa kupya, na siku mpya ambayo hurejeshwa roho ndani yake, na watu hutawanyika ndani yake, na wanapumua katika asubuhi hii mpya aliyoiumba Mwenyezi Mungu; ili iwe shahidi kwa mwanadam, na ili ziwe nyakati zake mida yake ni hazina ya matendo yetu.
- Mahusiano kati ya kauli yake "Na kwako ndio mafikio" na kusemwa jioni, ni pale watakaporejea watu katika matendo yao na kutawanyika kwa kwenda katika masilahi yao na maisha yao, wanarejea katika nyumba zao, na wanadumishwa katika raha baada yakuwa wametawanyika, inamkumbusha kurejea kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka kwa hatima na marejeo na mafikio.