- Himizo la kutilia umuhimu wa kujifunza udhu na sunna zake na adabu zake, na kuzifanyia kazi.
- Ubora wa udhu, nakuwa hilo ni kafara ya madhambi madogo, ama makubwa ni lazima kufanya toba.
- Sharti za kutoka kwa madhambi ni kuukamilisha udhu na kuuleta bila mapungufu kama alivyobainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
- Kufutwa kwa madhambi katika hadithi hii kumefungamanishwa na kuyaepuka madhambi makubwa na kuyaombea toba, amesema Mtukufu: "Ikiwa mtayaepuka madhambi makubwa mnayokatazwa tutakusameheni makosa yenu" [An-Nisaa: 31].