Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufanyiana kwao upole, ni kama mfano wa kiwiliwili, kinapopata tabu kiungo kimoja vinaitana kwa ajili ya hicho kimoja viungo vyote kwa kukesha na maumivu
kutoka kwa Nu'man Bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake -: "Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufanyiana kwao upole, ni kama mfano wa kiwiliwili, kinapopata tabu kiungo kimoja vinaitana kwa ajili ya hicho kimoja viungo vyote kwa kukesha na maumivu".
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Ufafanuzi
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa inatakiwa kuwa hali ya waislamu baadhi yao kwa baadhi katika kupendeleana kheri na kuhurumiana na kusaidizana na kuteteana, na kuudhika kwa yale madhara yanayowafika, kama mfano wa kiwiliwili kimoja, kikiugua kiungo kimoja, mwili mzima unashiriki kwa kukesha na maumivu pia.
Hadeeth benefits
Ni lazima kuziheshimu haki za waislamu na kuhimiza kuwasaidia na kuhurumiana wao kwa wao.
Ni lazima kwa watu wa imani kuwe na mapenzi na kuteteana.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others