- Mizoga ya wanyama wa baharini ni halali, na makusudio ya mizoga: Ni wale wanyama wa ndani ya bahari waliokufa katika wale waliofia humo miongoni mwa wale ambao hawaishi isipokuwa ndani ya maji.
- Kumjibu muulizaji kwa majibu zaidi ya kile alichouliza kwa ajili ya kukamilisha faida.
- Maji yakibadilika ladha yake au rangi yake au harufu yake kwa kitu chochote twahara (safi) basi hayo yataendelea kubaki katika utwahara wake madam bado yako katika uhalisia wake, hata kama chumvi yake itazidi au joto lake au baridi yake na mfano wa hivyo.
- Maji ya Bahari yanaondoa hadathi kubwa na ndogo, (uchafu usioonekana kama janaba) na yanaondoa najisi iliyojitokeza katika kitu twahara, kama mwili, au nguo, na kinginecho.