- Anaweka sheria kwa kila mwenye kuamka kutoka usingizini apenge ili kuondoa athari za Shetani puani mwake, na endapo kama atatawadha, hapo amri ya kupenga itakuwa ni lazima.
- Kupenga ni katika faida kamili ya kupandisha maji puani; na kupenga kunatoa uchafu huo kupitia maji.
- Kufungamanisha na usingizi wa usiku pekee, kwa kuchukua kutoka katika tamko "Kulala" kwani kulala huwa hakuwi ila kwa usingizi wa usiku, kwa sababu ndio usingizi wa kulala muda mrefu na wa fofofo.
- Katika hadithi kuna dalili kuwa Shetani humgusa mwanadam pasina yeye kulihisi hilo.