Kutoka kwa Ummu Salama mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Watakuja watawala, mtaya...
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa tutatawaliwa na viongozi ambao tutayajua baadhi ya matendo yao kuwa yako sawa na yale yanayofahami...
Imepokelewa kutoka kwa Bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika utakuja kutokea uch...
Alieleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake yakuwa waislamu watatawaliwa na viongozi watakaohodhi na kujipendelea mali za waislamu na mambo mengine m...
Kutoka kwa Abdillah Bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- amesema: "Kila mmoja miongoni mwen...
Anaeleza Mtume rehema na amani zimfikie kuwa kila muislamu katika jamii anamajukumu anayoyasimamia na anayoyabeba, Imamu na kiongozi ni mchunga katika...
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema ndani ya nyumba yangu hii: "Ewe Mola...
Alimuombea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kila atakayesimamia jambo katika mambo ya waislamu liwe dogo au kubwa, sawa sawa usimamizi huu uwe ni...
Imepokewa Kutoka kwa Tamim Ad-dari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: "Dini ni nasaha" Tuka...
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dini imesimama katika misingi ya kutakasa nia (Ikhlas) na ukweli, ili itekelezwe kama alivyowajibi...
Kutoka kwa Ummu Salama mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Watakuja watawala, mtayajua baadhi ya matendo yao kuwa yanakwenda sawa na sheria, na mengine mtayakemea (kwa kuwa yako nje ya sheria) atakayelijua hilo ataepukana na dhima, na atakayekemea atasalimika, lakini atakayeridhia na akawafuata" Wakasema: Kwa nini tusiwapige vita? Akasema: "Hapana, (Msifanye hivyo) madam ni waislamu na wanasimamisha swala".
Imepokelewa kutoka kwa Bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika utakuja kutokea uchoyo na kujipendelea baada yangu na mambo msiyoyajua (uzushi)" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unatuamrisha nini? Akasema: "Mtekeleze haki ya wajibu kwenu, na mumuombe Allah haki yenu".
Kutoka kwa Abdillah Bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- amesema: "Kila mmoja miongoni mwenu ni mchunga hivyo ataulizwa kuhusu raia wake, kiongozi anayewaongoza watu ni mchunga naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mwanaume ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwake naye ndiye wa kuulizwa kuhusu wao, na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mja ni mchunga juu ya mali ya bosi wake, naye ndiye atakayeulizwa juu ya mali hiyo, tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ni mchunga na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake".
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema ndani ya nyumba yangu hii: "Ewe Mola wangu! Yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawatia tabu, basi naye mtie tabu, na yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawahurumia, basi naye mhurumie".
Imepokewa Kutoka kwa Tamim Ad-dari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: "Dini ni nasaha" Tukasema: Kwa ajili ya nani? Akasema: "Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kitabu chake, na Mtume wake, na kwa viongozi wa waislamu na watu wote."
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alisoma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Aya hii :{Yeye ndiye ambaye alikuteremshia kitabu hiki ndani yake kuna Aya muhkam -zilizo wazi- aya hizo ambazo ndiyo msingi wa kitabu hiki na zipo nyingine zinatatiza, wale ambao nyoyoni mwao kuna upotofu watafuata zile zenye kutatiza kwa kutaka kufitinisha na kutaka kujua uhakika wa maana yake, na hakuna ajuaye uhakika wa maana yake isipokuwa Mwenyezi Mungu, na wale wabobezi katika elimu wanasema tumeziamini zote zimetoka kwa Mola wetu na hawakumbuki isipokuwa wenye akili} (Al- imaraan 7) Anasema Aisha: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ikiwa utawaona wenye kufuata Aya zenye kutatiza basi hao ndiyo ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika aya"
Hadithi imepokelewa na Abii Said Alkhuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Yeyote miongoni mwenu atayeona jambo ovu na baya basi aliondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi kuliondoa kwa mkono wake basi aliondoe kwa ulimi wake, na ikiwa hawezi kuliondoa kwa ulimi basi na alichukie kutoka moyoni mwake, na kuchukia moyoni ni udhaifu wa imani".
Kutoka kwa Nuumaan bin bashiri Radhi za Allah ziwe juu yao, kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina), wakawa baadhi yao wako juu ya safina na wengine wako chini yake, na wakawa wale walioko chini yake wanapohitajia maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, wakasema: Lau kama tungetoboa katika sehemu yetu kitobo wala tusingewaudhi walioko juu yetu, ikiwa watawaacha watekeleze walilolikusudia wataangamia wote, na ikiwa watawashika na kuwazuia wataokoka na wataokoka wote".
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao, na atakayelingania katika upotofu atakuwa kwake na madhambi mfano wa madhambi ya yule aliyemfuata, halipunguzi hilo katika madhambi yao chochote".
Kutoka kwa Abuu Masoud Al-Answari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika kipandwa changu kimeangamia nakuomba msaada wa usafiri, akasema: "Sina uwezo" Mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi nitamuonyesha kwa mtu atakayeweza kumbeba, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake".
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema siku ya vita vya Khaibari: "Kesho nitampa bendera hii mtu ambaye Mwenyezi Mungu ataleta ushindi kupitia mikononi mwake, ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda." Akasema: Watu wakalala usiku kucha wakijadili hilo, ni nani kati yao atakayepewa! Palipopambazuka watu walikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake wote wakitaraji kuwa atapewa, akasema: “Yuko wapi Ally bin Abi Twalib?" pakasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, anaumwa macho, akasema: “Basi mtumieni mtu akamuite.” Akaletwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akamtemea mate machoni mwake na akamuombea, akapona kana kwamba hakuwa na maradhi, hivyo akampa bendera, na Ally akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nipigane nao mpaka wawe kama sisi? Akasema: “Songa mbele, mpaka utue kwenye uwanja wao, kisha uwaite kuja katika Uislamu, na uwafahamishe yale yaliyo wajibu juu yao katika haki za Mwenyezi Mungu kwake, Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako, hilo ni bora zaidi kwako kuliko ngamia wekundu."
Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakaye jifananisha na watu fulani basi na yeye ni miongoni mwao".