- Miongoni mwa faida za hadithi hii ni kuwa
- hadithi hii ni msingi katika kuweka wazi hatua na taratibu za kuuondoa uovu.
- Maamrisho ya kwenda hatua kwa hatua katika kukataza uovu, hatua zote hizo ni kwa mujibu wa uwezo wa mtu.
- Kukataza uovu katika dini ni mlango mpana sana suala hilo hakuna wakulikwepa, na hulazimishwa kila muislamu kufanya hivyo kwa kadiri ya uwezo wake.
- Kuamrisha mema na kukataza mabaya ni katika mambo yanayofungamana na imani, na imani kwa kawaida huzidi na kupungua.
- Ni sharti katika kukataza uovu: kuwa na elimu ya kuwa kitendo hicho ni uovu.
- Ni sharti katika kuondoa uovu: Usipelekee kutokea uovu mkubwa kuliko huo.
- Kukataza uovu kuna taratibu zake na masharti ambayo anapaswa muislamu kujifunza.
- Kukataza maovu kunahitajia siasa ya kisheria, na kuwa na ujuzi na elimu.
- Kutokuondosha uovu kwa moyo ni dalili ya udhaifu wa imani.