- Katika alama za utume wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kueleza kwake mambo yatakayotokea miongoni mwa ghaibu na yakatokea kama alivyoeleza.
- Haifai kuridhia uovu wala kushiriki ndani yake, na ni lazima kuukemea.
- Watakapozua viongozi mambo yanayokwenda kinyume na sheria haitakiwi kuwatii katika hilo.
- Kutofaa kujitoa chini ya viongozi wa waislamu; kwakuwa hilo linaambatana na madhara na umwagaji damu na amani kutoweka, kuvumilia uovu wa viongozi watenda maasi, na kusubiri juu ya kero zao, haya ni mepesi kuliko kuvunja amani na kumwaga damu.
- Swala ina nafasi kubwa, ndio inayotenganisha kati ya ukafiri na Uislamu.