- Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na msamaha wake na fadhila zake.
- Ubora wa tauhidi, nakuwa Mwenyezi Mungu anawasamehe madhambi pamoja na maasi wenye kumpwekesha.
- Hatari ya ushirikina nakuwa Mwenyezi Mungu hawasamehe washirikina.
- Amesema bin Rajab: Hadithi hii inakusanya sababu tatu za kusamehewa dhambi: Ya kwanza: Kuomba dua pamoja na matumaini, ya pili: Kutaka msamaha na kuomba toba, ya tatu: Kufa katika tauhidi.
- Hadithi hii ni katika yale anayoyasimulia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na inaitwa Hadithil Qudsi (tukufu) Hadithi ya kiuungu, na maneno yake na maana yake ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu ila hayana sifa za Qur'ani ambazo inasifika nazo kuliko kitu kingine chochote, kama vile kumuabudu Mwenyezi Mungu kupitia kisomo chake, na kuwa na twahara kwa ajili yake, na kutoa changamoto na miujiza na kadhalika.
- Dhambi zina aina tatu: Ya kwanza: Kumshirikisha Mwenyezi Mungu; Na dhambi hili haisamehe Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu amemharamishia Pepo". Ya pili: Ni mja kujidhulumu mwenyewe katika yale yaliyo kati yake na Mola wake Mlezi, kama madhambi na maasi; Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu huyasamehe hayo, na kuyaachilia mbali akitaka. Ya tatu: Ni madhambi ambayo Mwenyezi Mungu haachi chochote katika hayo, nayo ni dhulma ya waja wao kwa wao, hivyo ni lazima kulipiza kisasi.