- Kwa mwenye akili analazimika kufanya haraka kuomba toba, na asijiaminishe na adhabu za Mwenyezi Mungu andapo atakuwa katika dhulma.
- Mwenyezi Mungu kuwapa muda madhalimu na kutokuwaharakishia adhabu huko ni kuwaleta taratibu na ni kuwaongezea adhabu endapo hawatotubia.
- Dhulma ni katika sababu za Mwenyezi Mungu kuziangamiza umma.
- Anapouangamiza Mwenyezi Mungu mji huenda kukawa na watu wema ndani yake, hawa watafufuliwa siku ya Kiyama katika matendo mazuri waliokufa nayo, na haidhuru wao kukumbwa na adhabu.