- Muujiza wa wazi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwani wasifu huu bado unaendelea Alhamdulillaah, kwanzia zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake mpaka hivi sasa, na bado utaendelea mpaka ije amri ya Mwenyezi Mungu iliyotajwa katika hadithi.
- Fadhila za kuwa na msimamo katika haki na kuifanyia kazi, na himizo juu ya hilo.
- Kudhihiri kwa dini kuna aina mbili: Ima kudhihiri kwa hoja na ubainifu na uwazi, na ima kudhihiri kwa dola na mhimili, na kudhihiri kulikobakia ni kwa hoja na ubainifu; kwa sababu hoja ya Uislamu ni Qur'ani, nayo iko wazi na inavitawala vitabu vingine visivyokuwa hiyo, lakini aina ya pili ya kudhihiri, ni kudhihiri kwa nguvu ya dola na mhimili, na hii inategemea kulingana na imani na kuwa na nguvu katika ardhi.