- Amri ya kusuhubiana na wema na kuwachambua, na katazo la kusuhubiana na watu wabaya.
- Ametajwa rafiki badala ya ndugu; Kwa sababu wewe ndiye unayemchagua rafiki, lakini ndugu na jamaa, huna chaguo.
- Kumchukua mtu kuwa rafiki lazima kuanze na kutafakari.
- Mtu huiimarisha dini yake kwa kusuhubiana na waumini na huidhoofisha kusuhubiana na watu waovu.