- Miongoni mwa sababu za kuingia katika matamanio ni shetani kuyapamba maovu na machafu, mpaka nafsi inayaona kuwa ni mazuri na kisha kuyaelekea.
- Amri ya kujitenga mbali na matamanio yaliyoharamishwa; kwa sababu hayo ni njia ya kuelekea motoni, na kuvumilia juu ya kero; kwani ni njia ya kuelekea Peponi.
- Ubora na fadhila za kupigana na nafsi na kuwa na bidii katika ibada na kuvumilia kero na tabu zinazo zizunguka ibada.