Ufafanuzi
Amesema Bin Masoud: Ametuhadithia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake naye ni mkweli kwenye maneno yake, na mwenye kukubaliwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemkubali, Amesema: Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake, na jambo hilo ni kuwa mtu akimuingilia mke wake basi yale manii yake yaliyosambaa hukusanywa kwenye tumbo la mwanamke kwa muda wa siku arobaini yakiwa ni tone la manii, Kisha hubadilika na kuwa pande la damu nzito iliyoganda, haya hufanyika katika arobaini ya pili, Kisha hubadilika kuwa pande la nyama, nacho ni kipande cha nyama chenye ukubwa wa kuweza kutafunwa, na mabadiliko haya ni katika arobaini ya tatu, Kisha Mwenyezi Mungu hulitumia pande hilo la nyama Malaika, kisha hulipulizia ndani yake roho baada ya kuisha siku arobaini za tatu, Na huamrishwa Malaika aandike maneno manne, nayo ni: Riziki yake, nacho ni kiwango ambacho atakipata miongoni mwake ni neema katika umri wake, Na pia huandikwa wakati wake, nao ni muda wa kubakia kwake Duniani, Na matendo yake, yatakuwa ni yapi? Na je atakuwa muovu au mwema. Kisha akaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yawezekana mtu akafanya matendo miongoni mwa matendo ya watu wa peponi, na yakawa matendo yake ni mazuri, yaani kwenye muonekano wa watu, na akabakia hivyo mpaka inakuwa kati yake na Pepo ni kiasi cha mkono, yaani kiasi kilichobaki kati yake mpaka kuifikia pepo ni kidogo sana kama vile ambavyo mtu amebakiza nafasi kati yake na ardhi kiasi cha mkono, mara Kitabu kinamtangulia na kile alichopangiwa, na wakati huo anafanya matendo ya watu wa motoni na akaandikiwa kuwa huo ndio mwisho wake na akaingia motoni; Kwa sababu sharti la kukubaliwa matendo yake ni kudumu katika matendo hayo na wala asibadilishe, na watu wengine wapo wenye kufanya matendo ya watu wa motoni mpaka mtu anakaribia kuingia motoni, mpaka inakuwa kati yake na kuingia motoni ni kiasi cha urefu wa mkono, basi kikamtangulia kitabu na alichopangiwa hivyo akafanya matendo ya watu wa peponi na akaingia peponi.