- Ubora wa kumtegemea Mwenyezi Mungu, nakuwa ni katika sababu kubwa ambazo huvuta riziki.
- Kumtegemea Mwenyezi Mungu hakupingani na kufanya sababu, kwani kaeleza kuwa kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa uhakika hakupingani na kutoka asubuhi na kurudi jioni katika kutafuta riziki.
- Sheria kutilia umuhimu matendo ya moyo; kwa sababu kutegemea ni katika matendo ya moyo.
- Kutegemea sababu pekee ni mapungufu katika dini, na kuacha kufanya sababu ni mapungufu ya akili.