- Kukemea uovu wakati wa kuuona na kutochelewa katika hilo, madam hakuna madhara makubwa katika hilo.
- Adhabu siku ya Kiyama itatofautiana kulingana na ukubwa wa dhambi.
- Kupiga picha za viumbe hai ni katika madhambi makubwa.
- Miongoni mwa hekima za kuharamishwa kupiga picha za viumbe hai ni kufafanisha vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu, sawa sawa mpigaji awe kakusudia kufananisha au hakukusudia hivyo.
- Sheria imetilia umuhimu juu ya kuhifadhi mali kwa kuitumia katika matumizi mengine baada ya kuitoa katika matumizi ya haram.
- Katazo la kutengeneza picha za viumbe hai kwa umbile lolote lile litakalokuwa, hata kama litakuwa ni dhalili.