Ufafanuzi
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka amesema kuwa amejiharamishia dhulma juu ya Nafsi yake, na akaifanya dhulma kuwa haramu baina ya waja wake, hivyo mtu asimdhulumu yeyote, Nakuwa viumbe wote wamepotea katika njia ya haki isipokuwa kwa uongofu wa Mwenyezi Mungu na taufiki yake, na atakayemuomba Mwenyezi Mungu uongofu basi atamuafikisha na atamuongoza, Nakuwa viumbe wote ni mafukara kwa Mwenyezi Mungu, wote ni wahitaji kwake katika haja zao zote, na atakayemuomba Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamtimizia haja zake na atamtosheleza, Nakuwa wao hutenda dhambi usiku na mchana, na Mwenyezi Mungu Mtukufu husitiri na husamehe pale mja anapomuomba msamaha, Nakuwa wao hawawezi kumdhuru Mwenyezi Mungu au kumnufaisha kwa chochote, Nakuwa wao lau kama wangelikuwa katika uchamungu wa moyo wa mtu mmoja, uchamungu wao usingeongeza chochote katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu, Na lau kama wangelikuwa katika uovu wa moyo wa mtu mmoja, uovu wao usingepunguza chochote katika Ufalme wake; kwa sababu wao ni madhaifu na mafakiri na ni wahitaji kwake kwa kila hali na kwa nyakati zote na mahala popote, na yeye ni mkwasi na utakasifu ni wake. Na lau kama wangelisimama mahala pamoja binadamu wao na majini wao, wa mwanzo wao na wa mwisho wao, wakimuomba Mwenyezi Mungu, akampa kila mmoja miongoni mwao ombi lake, hilo lisingepunguza chochote katika vile vilivyoko kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa ni kama mfano wa sindano inapoingizwa Baharini kisha ikatolewa, Bahari kamwe haipungukiwi na kitu, na hii ni kwa sababu ya ukamilifu wa utajiri wake Mtukufu.
Nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anayahifadhi matendo ya waja na kisha anawatunzia, kisha anawatimizia malipo siku ya Kiyama, atakayekuta malipo ya matendo yake yakiwa ni kheri basi na amshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuafikisha kwake katika kumtii, na atakayekuta malipo ya matendo yake ni kinyume na hivyo basi asilaumu ila nafsi yake yenye kuamrisha maovu iliyompelekea katika hasara.