- Sunna ya kutoa salamu kwa mujibu wa yaliyokuja katika hadithi, mtembea kwa miguu anapomsalimia aliyepanda kipando, na wengineo katika hao waliotajwa, inafaa, lakini ni kwenda kinyume na kilicho bora zaidi.
- Kutoa salamu kwa namna iliyokuja katika hadithi ni katika sababu za mapenzi na kujenga umoja.
- Wakiwa wanalingana na wako sawa katika hayo yaliyotajwa, basi mbora wao ni yule atakayeanza kwa salamu.
- Ukamilifu wa sheria hii katika kubainisha yote anayoyahitaji mwanadam.
- Kufundisha adabu za salamu na kumpa kila mwenye haki haki yake.