- Uwajibu wa kumpenda Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na kutanguliza mapenzi yake kuliko mapenzi ya viumbe wote.
- Katika alama za ukamilifu wa mapenzi: Ni kuzitetea sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kutoa nafsi na mali katika hilo.
- Kumpenda Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kunaendana na kumtii katika yale aliyoyaamrisha na kumsadikisha katika yale aliyoyaeleza na kuyaepuka yale aliyoyakataza na kuyakemea, na kumfuata na kuacha uzushi.
- Haki ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kubwa na ni ya mkazo kuliko watu wote; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa sababu ya sisi kuongoka kutoka katika upotevu na kutuokoa na moto na kufuzu kuipata Pepo.