- Kutofautiana ukubwa kwa madhambi, kama ambavyo matendo mema yanazidiana katika ubora.
- Dhambi kubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha kumuua mtoto kwa kuchelea kula naye, kisha kumzini mke wa jirani yako.
- Riziki iko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, na amechukua jukumu -Aliyetakasika- la kuwaruzuku viumbe.
- Ukubwa wa haki ya jirani, nakuwa kumuudhi ni dhambi kubwa kuliko kumuudhi mwingine.
- Muumba ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa yeye peke yake asiye na mshirika wake.