- Katazo la kuziacha nyumba bila ya kumuabudia Allah Mtukufu ndani ya majumba hayo.
- Katazo la kufunga safari kwa ajili ya kuzuru kaburi la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-; kwani yeye aliamrisha kumuombea rehema juu yake na akaeleza kuwa zinamfikia, bali hufungwa safari kwa kuukusudia msikiti pekee na kusali ndani yake.
- Uharamu wa kulifanyia matembezi kaburi la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni sikukuu, kwa kukithirisha kulizuru kwa namna maalum na kwa nyakati maalum, na vile vile ziara ya kaburi lolote.
- Utukufu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa Mola wake, kwa kuwekwa sheria ya kumtakia rehema kwa kila zama na kila mahali.
- Kiasi kwamba katazo la kuswali makaburini limepitishwa kwa maswahaba; kwa ajili hii alikataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- majumba kufanywa kuwa kama makaburi hakusaliwi ndani yake.