- Kuitukuza Sunna kama inavyotukuzwa Qur'ani tukufu na kuhukumu kwayo.
- Kumtii Mtume ndiyo kumtii Mwenyezi Mungu, na kumuasi Mtume ndiyo kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kuthibitika kuwa Sunna ni hoja, na jawabu kwa mwenye kuikataa Sunna au kuipinga.
- Na mwenye kuipinga Sunna na kudai kuwa Qur'ani pekee yamtosha, basi mtu huyo atakuwa kavipinga vyote viwili, na ni muongo kwa kudai kwake kuifuata Qur'ani.
- Miongoni mwa alama za utume wake Rehema na amani ziwe juu yake-, ni kutoa taarifa ya kitu kuwa kitatokea mbeleni na hutokea kama alivyotoa taarifa.