- Uharamu wa kufuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au mifugo au mazao.
- Kuwa na picha ni miongoni mwa mambo maovu ambayo Malaika huchukizwa nayo, na kuwepo kwake mahali hapo ni sababu ya kunyimwa huruma, na hivyo hivyo kwa mbwa.
- Malaika ambao hawaingii ndani ya nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha ni Malaika wa rehema, lakini kwa walinzi na wengine ambao wana kazi kama Malaika wa mauti, wanaingia kila nyumba.
- Uharamu wa kutundika picha za viumbe wenye roho juu ya kuta na kwingineko.
- Amesema Al-Khattwabi: Bali Malaika hawaingii ndani ya nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha, jambo linalopelekea uharamu wa kumiliki mbwa na picha, ama mbwa wasiokuwa haramu ni kama vile mbwa wa kuwinda, wa mazao, na wa mifugo, na picha zinazotumika katika zulia, mito, na vitu vingine, kwa kukanyagwa na kudhalilishwa hizi haziwezi kuwa sababu ya kuzuia Malaika kuingia.