- Ulazima wa kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutahadhari na riyaa.
- Huruma yake kubwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya umma wake na pupa yake ya kutaka kuwaongoza na kuwapa kwake nasaha.
- Ikiwa hii ndio hofu yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akizungumza na Masahaba ambao ndio watukufu kwa watu wema, basi hofu kwa wale wataokuja baada yao ni kubwa zaidi.