- Hadithi hii ni miongoni mwa yale anayayopokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithil Qudsi au Ilaahiy, nayo ni ile ambayo lafudhi yake na maana yake inatoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa haina umaalum kama Qur'ani ambapo Qur'ani imesifika nao tofauti na maneno mengine, ikiwemo kutumika kisomo chake kama ibada, nakuwa msafi kabla ya kusoma, na changamoto, sayansi zilizomo ndani yake, na mengine mengi.
- Katazo la kuwaudhi vipenzi wa Mwenyezi Mungu na himizo la kuwapenda, na kukiri ubora wao.
- Amri ya kuwafanyia uadui maadui wa Mwenyezi Mungu na uharamu wa kuwapenda.
- Atakayedai uwalii (Kupendwa na) Mwenyezi Mungu pasina kufuata sheria yake huyo ni muongo katika madai yake.
- Mapenzi ya Mwenyezi Mungu hupatikana kwa kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho.
- Miongoni mwa sababu za mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa mja na kujibu maombi yake, ni kutekeleza mambo ya sunna baada ya kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho.
- Ushahidi juu ya utukufu wa mawalii (Vipenzi wa Mwenyezi Mungu) na daraja zao za juu.