- Adhabu hii si maalum kwa kiongozi mkuu na wasaidizi wake, bali inajumuisha kila atakayepewa usimamizi na Mwenyezi Mungu kwa raia.
- Wajibu kwa kila atakayesimamia lolote katika mambo ya waislamu awanasihi, na ajitahidi kutimiza amana, na atahadhari na hiyana.
- Ukubwa wa majukumu kwa kila atakayewasimamia raia kwa umma au binafsi, sawa majukumu yawe madogo au makubwa.