- Katazo la kufuga mbwa na kusuhubiana nao, isipokuwa mbwa wa kuwinda au wa ulinzi.
- Malaika wanaojizuia kufuatana na msafara ni Malaika wa rehema, ama wale waandika matendo hao hawamwachi mtu akiwa nyumbani au safarini.
- Katazo la kengele; kwani ni zumari katika mazumari ya shetani, na kuna kujifananisha na Wakristo.
- Ni juu ya muislamu kujiweka mbali na yale yote yanayowaweka Malaika mbali naye .