- Kuwatii viongozi ni wajibu katika mambo yasiyomuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kuna tahadhari kubwa kwa aliyetoka katika utiifu kwa kiongozi, na akasambaratisha umoja wa waislamu, akifa katika hali hii, atakuwa amekufa katika njia ya watu wajinga.
- Katika hadithi kuna katazo la kupigana vita kwa sababu ya ubaguzi.
- Ulazima wa kutimiza makubaliano.
- Katika utiifu na kushikamana na umoja kuna heri nyingi, na amani na utulivu, na hali kutengamaa.
- Katazo la kujifananisha na watu zama za ujinga.
- Amri ya kushikamana na umoja wa waislamu.