- Uharamu wa ukuhani, na kwenda kwa makuhani na kuwauliza mambo ya ghaibu.
- Mtu anaweza kunyimwa thawabu za ibada ikiwa ni adhabu kwake kwa kutenda kwake maasi.
- Yanaingia katika hadithi hii yanayoitwa nyota na kutazamia, na kusoma viganja na vikombe hata kama ni kwa kutaka kujua pekee; kwa sababu hiyo yote ni katika ukuhani na ni katika kudai kujua elimu ya ghaibu.
- Ikiwa haya ndiyo malipo ya mwenye kumuendea mpiga ramli, ni vipi malipo ya mpiga ramli mwenyewe?.
- Swala za siku arobaini zinaangukia katika kutokubalika, si wajibu kuzilipa lakini hazina thawabu ndani yake.