- Ni sunna kusema baada ya kuteremka Mvua: Tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na Rehema zake.
- Yeyote atakaye egemezea neema ya kuteremka Mvua na neema zingine katika Nyota kwa kuumbwa na kuwepo kwake basi mtu huyo ni kafiri aliyekufuru kufuru kubwa, ama yule atakayeegemeza kuwa Nyota ni sababu basi huyo amekufuru kufuru ndogo, kwa sababu Nyota siyo sababu ya kuteremka mvua kisheria wala kihisia.
- Nikuwa neema inakuwa ni sababu ya kukufuru endapo itakanushwa, na huwa ni sababu ya kuwa na imani endapo itashukuriwa.
- Kumekatazwa kusema kuwa: "Tumepata mvua kwa kuanguka Nyota fulani" hata kama yatakuwa makusudio yake ni wakati fulani (kama msimu wa masika); kwa kuzuia mlango wa shirki.
- Ni wajibu kuufungamanisha moyo na Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika kuleta neema na kuondosha matatizo.