- Kuilinda tauhidi na itikadi dhidi ya yale yenye kuzibomoa.
- Uharamu wa kutumia makombe ya kishirikina na hirizi na limbwata.
- Mtu kuamini katika mambo matatu haya kuwa yenyewe ndiyo sababu: Hii ni shirki ndogo; Kwa sababu hii ni kuyafanya yasiyokuwa sababu kuwa ni sababu, ama akiitakidi kuwa yananufaisha na kudhuru yenyewe hii ni shirki kubwa.
- Tahadhari ya kufanya sababu za kishirikina na zilizoharamishwa.
- Kumeharamishwa makombe na kuwa ni katika shirki isipokuwa yale yatakayokuwa kisheria.
- Ni lazima moyo ufungamane na Mwenyezi Mungu peke yake, kwake ndio hutoka madhara na manufaa peke yake asiyekuwa na mshirika, hakuna aletaye kheri isipokuwa Allah na hakuna azuiaye shari isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Ruqiya inayofaa ni ile iliyoambatana na sharti tatu: 1- Aitakidi kuwa ni sababu na wala haiwezi kunufaisha isipokuwa kwa idhini ya Allah. 2- Iwe kwa Qur'ani na majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake na dua za Mtume za kisheria. 3- Iwe kwa lugha inayofahamika, na wala isiambatane na matalasimu na mazingaombwe.