- Uharamu wa kuapa kumuapia asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikiwemo: Kuiapia amana, nakuwa hilo ni katika shirki ndogo.
- Amana inakusanya utiifu na ibada, na kuwekeza, na pesa tasilimu, na amana.
- Kiapo hakikubaliki ila kwa kuapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu au kwa jina miongoni mwa majina yake au kwa sifa katika sifa zake.
- Amesema Al-Khattwabi: Hadithi inaonekana kuwa karaha hapa ni kwa sababu aliamrisha aape kwa Allah na kwa sifa zake, na amana si katika sifa zake, bali ni amri katika amri zake, na ni faradhi katika faradhi zake, wakakatazwa hilo kwakuwa ndani yake kuna kuifanya amana kuwa sawa na majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka na sifa zake.