/ Atayeapa kinyume na Mwenyezi Mungu basi atakuwa amekufuru au kafanya ushirikina

Atayeapa kinyume na Mwenyezi Mungu basi atakuwa amekufuru au kafanya ushirikina

Imepokelewa Kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- yakwamba yeye alimsikia mtu mmoja akisema: Hapana! naiapia Al-ka'aba, akasema bin Omar: Hakuapiwi kinyume na Mwenyezi Mungu, kwani mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atayeapa kinyume na Mwenyezi Mungu basi atakuwa amekufuru au kafanya ushirikina"

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na majina yake na sifa zake basi atakuwa kamkufuru Mwenyezi Mungu au kafanya ushirikina; kwa sababu kiapo humaanisha kutukuzwa mwenye kuapiwa, na utukufu ni wa Allah pekee; hakuapiwi ila kwa Allah na majina yake na sifa zake kutakasika machafu ni kwake. Na kiapo hiki ni katika shirki ndogo; lakini ikiwa muapaji atakitukuza alichokiapia kama anavyomtukuza Allah Mtukufu au zaidi; basi hapo itakuwa katika ushirikina mkubwa.

Hadeeth benefits

  1. Nikuwa kutukuza kwa kiapo ni katika haki za Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- hakuapiwi ila kwa Allah na majina yake na sifa zake.
  2. Pupa ya Masahaba katika kuamrisha mema na kukataza maovu, hasa hasa uovu unapokuwa unahusiana na ushirikina mkubwa au kufuru.