- Uwajibu wa kumtegemea Allah na kuamini hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake, na kuharamishwa kwa imani za mikosi na nuksi na uchawi na ukuhani, au kuwauliza wenye mambo hayo.
- Kudai kujua elimu ya ghaibu ni katika shirki inayopingana na tauhidi.
- Uharamu wa kuwasadikisha makuhani na kuwaendea, na vinaingia hapa kusoma viganja na kusoma yaliyoandikwa kwenye vikombe na kutazamia nyota na, hata kama ni kwa kutaka kujua.