- Ibada zote zimejengeka juu ya yale yalikuja katika Qur'ani na Sunna, hatutakiwi kumuabudu Allah Mtukufu isipokuwa kwa sheria aliyoiweka na si kwa uzushi na mambo ya kutungwa.
- Dini haiendi kwa rai na kutazama lipi zuri, bali inakwenda kwa kumfuata Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
- Hadithi hii ni ushahidi wa kukamilika dini.
- Uzushi ni kila kilichozushwa katika dini na hakikuwepo katika zama za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na Masahaba zake katika itikadi (Aqida) au kauli au amali yoyote.
- Hadithi hii ni msingi katika misingi ya Uislamu, nayo ni sawa na mzani kwa matendo, kama ambavyo kila amali ambayo haikukusudiwa kupata radhi za Allah Mtukufu, mfanyaji wake hana thawabu ndani yake, hivyo hivyo kila amali ambayo haitakuwa samabamba na yale aliyokuja nayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- basi hiyo itarejeshwa kwa mfanyaji wake.
- Uzushi uliokatazwa ni ule unaokuwa katika mambo ya dini na si ya kidunia.