- Kuthibitisha uombezi wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Akhera, nakuwa hautokuwa ila kwa watu wa tauhidi.
- Uombezi wake -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kuomba kwake kupitia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yule atakaye stahiki Moto katika watu wa tauhidi ili asiuingie, na aliyeuingia atoke.
- Ubora wa neno la tauhidi lililotakasiwa nia kwa ajili ya Allah Mtukufu na athari zake kubwa.
- Kulihakikisha neno la tauhidi kunakuwa kwa kujua maana yake, na kufanyia kazi makusudio yake kwa namna inavyotakikana.
- Ubora wa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-, na pupa yake juu ya elimu.