- Ubora wa Tauhidi na kuwa yeyote atakaye kufa hali yakuwa ni muumini wa kweli hajamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi.
- Hatari ya ushirikina, nakuwa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni.
- Wafanya maasi wale wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu wapo chini ya utashi wa Mwenyezi Mungu, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe, kisha mafikio yao yatakuwa peponi.