- Kutamka Laa ilaaha illah llaah, na kuyapinga yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, ni sharti la kuingia katika Uislamu.
- Maana ya (Laa ilaaha illa llaah) ni kupinga kila kinachoabudiwa kinyume na Allah yakiwamo masanamu na makaburi na mengineyo, na kumpwekesha yeye Mtukufu kwa ibada.
- Atakayeileta tauhidi na akashikamana na sheria zake kwa dhahiri ni wajibu kujizuia kutomtendea baya mpaka yabainike yanayokwenda kinyume na hilo.
- Uharamu wa kula mali ya Muislamu na kumwaga damu yake na kuvunja heshima yake ila kwa haki.
- Hukumu duniani ni kwa yale yanayoonekana, na akhera ni katika nia na makusudio.