- Unyenyekevu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kumpakiza kwake Muadhi nyuma ya mnyama wake.
- Njia ya ufundishaji wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba alirudia rudia wito kwa Muadhi ili akaze usikivu wake kwa yale atayoyazungumza.
- Katika sharti za shahada: Ya Kushuhudia kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni awe msemaji wake ni mkweli na yakini, asiwe muongo au na shaka.
- Watu wa tauhidi hawatokaa milele katika moto wa Jahannam, hata kama watauingia kwa sababu ya madhambi yao; watatolewa baada ya kusafishwa.
- Fadhila za shahada mbili kwa atakayezisema akiwa mkweli.
- Kufaa kuacha kuzungumza baadhi ya mazungumzo katika baadhi ya hali, yatakapoambatana na madhara.