- Kumewekwa wazi haki za Mwenyezi Mungu ambazo amewajibisha kwa waja wake, nazo ni kumuabudu yeye, na wasimshirikishe na kitu chochote.
- Kumewekwa wazi haki ya waja kwa Mwenyezi Mungu ambayo ameiwajibisha yeye mwenyewe kwa fadhila zake na neema zake, na haki hiyo ni kuwaingiza peponi, na kutowaadhibu.
- Katika hadithi hii kuna bishara njema na kubwa kwa wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, wale ambao hawamshirikishi Mwenyezi Mungu Mtukufu na kitu chochote, na kuwa mafikio yao ni kuingia peponi.
- Alihadithia Muadhi hadithi hii kabla ya kufa kwake; kwa kuogopea kuingia kwenye madhambi ya kuficha elimu.
- Kuna tahadhari ya kuacha kueneza baadhi ya hadithi kwa baadhi ya watu kwa kuogopea mtu kutofahamu maana yake; na hofu hiyo ni kwa yule ambaye hana matendo wala hayupo kwenye sheria miongoni mwa sheria.
- Wafanyaji maasi wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu wapo chini ya utashi wa Mwenyezi Mungu, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe, kisha mafikio yao yatakuwa peponi.