- Himizo la kuwa na Ikhlasi (kutakasa nia) kwani Mwenyezi Mungu hakubali katika matendo isipokuwa yale yatakayokusudiwa kupata radhi zake.
- Matendo ambayo hutumika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwayo, akiyafanya muislamu mtu mzima kwa njia ya mazoea hawezi kuwa na thawabu juu yake, mpaka akusudie kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo hayo.