- Sunna ya dua hii wakati wa kuingia msikitini na wakati wa kutoka.
- Zimetengwa rehema wakati wa kuingia, na fadhila wakati wa kutoka: Kwani mwenye kuingia hushughulika na yale yanayomkurubisha kwa Allah na katika Pepo yake ikawa ni bora ataje rehema, na anapotoka hutembea katika Ardhi kwa ajili ya kutafuta fadhila za Allah miongoni mwa riziki, ikawa ni bora kwake kutaja fadhila.
- Dua hizi husomwa wakati wa kutaka kuingia msikitini, na wakati wa kutaka kutoka.