- Kutaka ulinzi ni ibada, nako ni kule kunakokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu au kwa majina yake na sifa zake.
- kufaa kutaka ulinzi kupitia majina ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu majina hayo ni sifa miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, kinyume na kutaka ulinzi kwa kiumbe yeyote kwani hii ni shirki.
- Ubora wa dua hii ni baraka zake.
- Kujikinga kupitia adhkari ni sababu ya mja kulindwa na shari.
- Kubatilika kutaka ulinzi kutoka kwa asiyekuwa Allah miongoni mwa Majini na wachawi na matapeli na wengineo.
- Sheria ya dua hii kusomwa na mwenye kushuka mahali nyumbani au safarini.